Wednesday, November 28, 2012
HAKIKA.............
Mungu ni yule yule jana leo na hata milele!ni yeye aliyewapitisha wana wa Israel katika bahari ya shamu ingawa kuna kipindi wana wa israel walikata tamaa lakini bado MUNGU alibaki kuwa MUNGU!
kinachotakiwa ni kutokukata tamaa kweli hapa duniani kuna wakati unaweza ukapata majaribu ambayo yanaonekana hayawezekani kwa khali ya kibinadamu!ila neno la MUNGU linasema kwa
''''''' MUNGU YOTE YAWEZEKANA!
jamani HUYU MUNGU NI MWEMA NA ANATUPENDA SANA anasema sitakuacha wala sitakupungukia kabisa!tumtafuteni BWANA MAADAMU APATIKANA TUMWITENI YEYE MAANA YUHAI''''''''''
'''USIKATE TAMAA, IPO NJIA''''
''''Yawezekana unapita katika magumu na unaona hakuna njia tena NA unakata tamaa.
Umefika mahali na unasema siwezi kupata kazi tena, hii kazi siwezi tena, haya mahusiano yamenishinda,
hii NDOA imenishinda, hawa watoto wamenishinda, hii shule imenishinda, siwezi kujenga, hii biashara imekufa, siwezi kuwa na biashara tena, n.k…….
''''IPO NJIA....... Inaweza isiwe rahisi na inaweza iwe ndefu. Hata kama panaonekanika kama hakuna njia, kwa Mungu kuna njia wakati wote. Na kama Yesu ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako, basi Roho Mtakatifu anaishi ndani yako. Ubunifu wote ulimwenguni upo ndani yake, na kwa kuwa yupo ndani yako, ubunifu utaupata. Roho Mtakatifu ana uwezo wa kukupa fikra ambazo hujawahi kuwa nazo na kukuonyesha njia ya kufanya vitu ulivyofikiri hutakaa uwezekufanya.''''
Badala ya kukumbatia magumu, inatubidi kuelekeza mawazo yetu kwa Mungu na tujue ya kwamba yeye yupo kwa ajili yetu na nguvu yake ipo kazini kwa ajili yetu. Tufike mahali tuone ya kwamba iwepo njia au isiwepo Yesu ndiye njia, Roho mtakatifu yupo ndani yangu na nitaipata njia ya kutokea tuu.
Mungu ametuahidi katika Isaya 43:19 akisema “tazama, nitatenda tendo jipya; sasa litachipuka, je! Hamtalijua sasa? NITAFANYA NJIA HATA JANGWANI, na MITO YA MAJI NYIKANI”. Katika injili ya yohana 14:16 Bwana Yesu alisema “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima”. Yeye ndiye njia, atakusaidia kuiona njia pale inapoonekana kama hakuna njia. Pia katika Wakorinto wa kwanza 10:13 tunafundishwa ya kwamba “Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya mwanadamu; ila Mungu ni mwaaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili”.
Kumbuka Mungu aliwafanyia wana wa Israel njia kavu baharini (soma Kutoka 14), walivushwa mto Jordan (soma Joshua 3). Tazama Injili ya Luka 1:37 “kwa kuwa hakuna neon lisilowezekana kwa Mungu”
Kwa maneno mengine ni kwamba, wakati wote na katika hali yeyote, Mungu ana njia kwa ajili yetu kama tukiitafuta, tukiwa na subira na kama tutakataa kukata tamaa.........
Subscribe to:
Posts (Atom)