'''USIKATE TAMAA, IPO NJIA''''

''''Yawezekana unapita katika magumu na
unaona hakuna njia tena NA unakata tamaa.
Umefika mahali na unasema
siwezi kupata kazi tena, hii kazi siwezi tena, haya mahusiano
yamenishinda,
hii NDOA imenishinda, hawa watoto wamenishinda, hii shule
imenishinda, siwezi kujenga, hii biashara imekufa, siwezi kuwa na
biashara tena, n.k…….
''''IPO NJIA.......
Inaweza isiwe rahisi na inaweza iwe ndefu. Hata kama panaonekanika kama
hakuna njia, kwa Mungu kuna njia wakati wote. Na kama Yesu ni Bwana na
Mwokozi wa maisha yako, basi Roho Mtakatifu anaishi ndani yako. Ubunifu
wote ulimwenguni upo ndani yake, na kwa kuwa yupo ndani yako, ubunifu
utaupata. Roho Mtakatifu ana uwezo wa kukupa fikra ambazo hujawahi kuwa
nazo na kukuonyesha njia ya kufanya vitu ulivyofikiri hutakaa
uwezekufanya.''''
Badala ya kukumbatia magumu, inatubidi
kuelekeza mawazo yetu kwa Mungu na tujue ya kwamba yeye yupo kwa ajili
yetu na nguvu yake ipo kazini kwa ajili yetu. Tufike mahali tuone ya
kwamba iwepo njia au isiwepo Yesu ndiye njia, Roho mtakatifu yupo ndani
yangu na nitaipata njia ya kutokea tuu.
Mungu ametuahidi katika Isaya 43:19
akisema “tazama, nitatenda tendo jipya; sasa litachipuka, je! Hamtalijua
sasa? NITAFANYA NJIA HATA JANGWANI, na MITO YA MAJI NYIKANI”. Katika
injili ya yohana 14:16 Bwana Yesu alisema “Mimi ndimi njia, na kweli, na
uzima”. Yeye ndiye njia, atakusaidia kuiona njia pale inapoonekana kama
hakuna njia. Pia katika Wakorinto wa kwanza 10:13 tunafundishwa ya
kwamba “Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya
mwanadamu; ila Mungu ni mwaaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita
mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea,
ili mweze kustahimili”.
Kumbuka Mungu aliwafanyia wana wa Israel
njia kavu baharini (soma Kutoka 14), walivushwa mto Jordan (soma Joshua
3). Tazama Injili ya Luka 1:37 “kwa kuwa hakuna neon lisilowezekana kwa
Mungu”
Kwa maneno mengine ni kwamba, wakati
wote na katika hali yeyote, Mungu ana njia kwa ajili yetu kama
tukiitafuta, tukiwa na subira na kama tutakataa kukata tamaa.........
No comments:
Post a Comment